Home » Afisa Wa Polisi wa Kikosi Cha Usalama Cha Ruto Ajipiga Risasi

Afisa Wa Polisi wa Kikosi Cha Usalama Cha Ruto Ajipiga Risasi

868 00

Afisa mmoja wa polisi aliyehusika na usalama wa naibu rais alijiua akiwa nyumbani kwake Juja, Kaunti ya Kiambu.

Konstebo Samuel Ngatia, mwanachama wa kikosi cha usalama cha Naibu Rais William Ruto, alifariki Jumatatu asubuhi baada ya kujipiga risasi kichwani.

Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana.

Ripoti ya polisi iliyowasilishwa katika kituo cha polisi cha Hays huko Juja ilionyesha kuwa mwathiriwa alikuwa peke yake ndani ya nyumba ndani ya kambi ya kikosi cha Recce cha General Service Unit kwenye Barabara ya Kenyatta wakati wa tukio.

“Alitumia bastola yake na kujipiga risasi kichwani na matokeo ya awali kuonyesha kwamba risasi iliingia upande wa kulia na kutoka upande wa kushoto,” ripoti hiyo ilisema.

Bastola aina ya Jericho iliyokuwa na risasi 13 na trevor sub machine gun ikiwa na magazine mbili zilizokuwa na risasi 30 zilipatikana ndani ya nyumba hiyo.

Polisi pia walipata katriji mbili zilizotumika na kichwa kimoja cha risasi.

Timu ya wapelelezi kutoka Thika na Juja wanachunguza tukio hilo.